Virusi vya Corona: Wagonjwa 12 wapya wathibitishwa Kenya

Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya corona nchini kenya, imefikia 396 amesema katibu katika wizara ya afya Dkt. Rashid Aman.
Wizara ya afya imesema kwamba kati ya walipimwa, 12 wamethibitishwa kuambukizwa corona na kufikisha idadi hiyo kuwa 396.
Walioambukizwa, 7 wanatoka Mombasa, 3 Mombasa, Kitui 1 na Wajir 1. Kaunti ya Wajir hiki ni kisa chake cha kwanza cha virusi vya corona.
Kwa saa 24 zilizopita, wagonjwa 15 wamepona ikiwa ndio idadi ya juu tangu kutangazwa kwa virusi hivi nchini mno huku wale waliopona ikifikia 144 kwa ujumla. Aidha, vipimo 777 vimefanywa katika kipindi hicho ikifikisha jumla ya watu 20,268 walifanyiwa vipimo hadi sasa.
Upande wa jinsia 9 ni wanaume huku 3 wakiwa wanawake huku mdogo zaidi akiwa na umri wa mwaka mmoja unusu.
Aidha wawili wamethibitishwa kufa na kufikisha idadi hiyo kuwa 17.
Katibu wa wizara hiyo Dkt. aetuma risala za rambirambi kwa familia za waathirika. Amekiri kwamba vita hii haijakuwa rahisi lakini amewataka raia kuendelea kuwa imara na kutii kanuniz zilizowekwa.
"Tunapoingia mwezi mwengine, tuendelee kuwa imara katika kukabiliana na virusi vya corona," amesema.
Coronavirus
Banner
Mkurugenzi wa Afya ya Umma Patrick Amoth, kwa mara nyengine tena amesema kwamba utabiri wa vile ugonjwa huo unaweza kutuathiri unategemea na matukio wala haimaanishi kwamba hivyo ndivyo itakavyokuwa.
Wakati huohuo, Bwana Aman pia ameelezea matumaini ya kwamba huenda hali mpaka kidogo ikaanza kulegezwa baada ya kufikiwa na itifaki iya kufuatwa na
Ikiwa ni pamoja na madereva kupimwa mpakani.
Pia wizara hiyo imeahidi taarifa za kina kuhusu matumizi ya fedha za benki ya Dunia.
Wiki jana, Mkurugenzi wa Afya ya Umma Patrick Amoth, alisema kwamba wizara yake inajaribu kuharakisha mchakato wa kuwapima watu waliowasilishwa katika vituo vya karantini baada ya kukiuka amri ya kutotoka nje kuanzia saa moja usiku hadi saa kumi na moja alfajiri iliotolewa na serikali na baada ya kupimwa wataruhusiwa kwenda nyumbani ili kujitenga.
Wizara ya afya iliwahi kuwashukuru wakenya kwa kuchukulia mwongozo wa kuosha mikono na umakini mkubwa na kuwaomba Wakenya kutii sheria.
Ila illijitokeza kwamba Wakenya wengi wanategemea sana vitakasa mikono badala ya kutumia maji na sabuni.
Patrons will be expected to wear face masks, sanitise and sit 1.5 metres apart
Image captionWahudumu watahitajika kuvaa barakoa, kutumia vitakasa mikono na kutokaribiana umbali wa mita 1.5
Masharti ya kuzingatiwa kwa migahawa kufunguliwa
Pia wizara ya afya imeweka wazi kwamba migahawa inayotaka kufungua tena, lazima itimize vigezo na kupata cheki kutoka kwa wizara hiyo.
Mwanzo wa wiki hii, wizara hiyo ya afya ilitangaza kwamba itaruhusu migahawa kufunguliwa tena ila kwa masharti.
Migahawa itafunguliwa kuanzia saa 11 asubuhi na 10 jioni.
Watakaoingia kuhudumiwa watahitajika kufuata utaratibu uliopo wa kunawa mikono, kutumia vitakasa mikono na kuvaa barakoa kama kawaida. Hatua ya kutokaribiana itaendelea kutekelezwa umbali wa mita 1 baina ya mtu mmoja hadi mwengine.
Wizara hiyo imetoa agizo la watu wote wanaoingia migahawani kupimwa kiwango cha joto na kuruhusiwa tu kuingia ikiwa litakuwa chini ya nyuzi 37.5 na mgahawa husika kuarifu wizara mara moja kuhusu mtu atakayepatikana akiwa na kiwango ha juu zaidi ya hicho, kwa kupiga simu kupitia nambari 719 ili kupata mwongozo zaidi.
Lakini watakaoruhusiwa kutoa huduma ni wale watakaokuwa wamepimwa pekee.
Pia kulingana na wizara ya afya, katika migahawa hiyo, huduma ya kujiwekea chakula bado imesitishwa.

Post a Comment

0 Comments