Wafanyakazi 15 katika taasisi ya saratani mjini Cairo waambukizwa corona

Wafanyakazi 15 wa afya katika hospitali kuu ya saratani nchini Misri wamegundulika kuambukizwa virusi vya corona, na kuwekwa chini ya karantini.

Meneja wa taasisi ya taifa ya saratani iliyoko chini ya chuo kikuu cha Cairo, Daktari Reem Emad amesema jumla ya madaktari watatu na wauguzi 12 wamethibitika kuwa na COVID-19.

Msemaji wa chuo kikuu cha Cairo Mahmoud Alameldeen amesema, taasisi hiyo itawapokea wagonjwa wa dharura pekee.

Hadi kufikia hivi sasa Misri imeripoti kesi 985 za corona na vifo 66. Mamlaka nchini humo zilianzisha marufuku ya wiki mbili ya kutotoka nje tangu Machi 25, katika juhudi za kukabiliana na kuenea kwa maambukizi.

Shule, vyuo, kumbi za starehe na sinema, makanisa na misikiti vyote vimefungwa.

Post a Comment

0 Comments