Wagonjwa wapya wa Corona ni kutoka DSM, Mwanza na Zanzibar

Waziri Ummy Mwalimu amethibitisha kuwepo kwa watu wanne walioambukizwa Virusi vya Corona amesema watu hao wamepatikana DSM, Mwanza , Kaskazini Magharibi mwa Tanzania na visiwani Zanzibar na kufanya idadi ya walio na maambukizi kufikia 24 tangu kuanza kwa ugonjwa huo nchini Tanzania.
Miongoni mwao wagonjwa wapya wa Tanzania bara ni mwanaume mwenye miaka 41 raia wa Tanzania, mfanyabiashara na mkazi wa Mwanza aliyeingia nchini akitokea Dubai tarehe 24 mwezi Machi kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) na kuelekea Mwanza tarehe 29 Machi.


Post a Comment

0 Comments