Wanyama afunguka sababu za kujiunga na Montreal ya MLS

Kiungo wa Kenya aliyekuwa anacheza Tottenham Hotspurs ya Uingereza Victor Wanyma, amefunguka sababu za kuamua kujiunga na club ya Montreal Impact ya Ligi Kuu ya Marekani.

Wanyama ambaye aliondoka Tottenham kwa kumuomba kocha wa timu hiyo Jose Mourinho kutokana na kukosa nafasi ya kucheza, aliamua kujiunga na MLS licha ya kuwa na ofa zilizotoka vilabu vya Hispania na Italia.

Wanyama kaeleza kuwa aliyesaidia kuamua kwenda MLs ni kocha wa timu hiyo Thierry Henry lakini pia aliwauliza wachezaji wenzake wa kama Bojan Krkic ambaye anaichezea klabu hiyo.

”Wa kwanza kunishawishi ni Thierry Henry ambaye aliiweka wazi kabisa ni kiasi gani ananihitaji kucheza MLS, aliuza Montreal kwangu kirahisi sana (kuisifia) pili niliongea na Luis Binks ambaye alikuwa akicheza Tottenham, Sapher Taider niliyewahi kucheza nae Southampton na Bojan Krkic wote waliniambia hii ni sehemu sahihi” - Wanyama

Post a Comment

0 Comments