Watu 50 waliotoroka karantini Kenya wasakwa


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa watu wote 50 waliotoroka kutoka kwenye kituo cha karantini cha watu wanaoshukiwa kuwa na virusi vya corona mjini Nairobi watakamatwa tena na kurejeshwa tena kwenye vituo hivyo ili waendelee kujitenga kiufuatia mlipuko wa Corona.

Akizungumza na kituo kimoja cha redio nchini Kenya, Bw. Kenyatta amesema: ''Tutawatafuta watu wote 50 waliotoroka kituo cha karantini na kuhakikisha wanajitenga kutokana na mlipuko wa Covid -19 wa virusi vya corona''.

Kauli hiyo ya rais wa Kenya inakuja baada video ya watu wasiojulika kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya ikionyesha watu wakitoroka kituo cha karantini katika Chuo cha mafunzo ya tiba cha Kenya (KMTC).

''Msako wa kuwakamata watu 50 waliotoroka karantini unaendelea,Wakenya waheshimu hatua za kukabiliana na Covid-19.'', alisema rais Kenyatta.

Watu hao walioonekana wakikwea ukuta wa jengo la Chuo hicho na kudondoka kwenye barabara ya Mbagadhi na kisha kuondoka kwa mwendo wa kasi na kuchangamana na wapitanjia wengine na baadae kutoweka.

Moja ya wodi ya kuwatenga wagonjwa katika hospitali ya Mbagathi Nairobi
Kituo cha Karantini katika kilikua na jumla ya watu 200 waliotengwa baada ya kubainika kuwa walikutana na watu waliokuwa na virusi vya corona pamoja na wale waliokiuka amri za kutotoka nje na kutosogeleana.

Inaaminiwa kuwa baadhi walitoroka Jumatatu usiku wakati mvua ilipokua inanyesha na waliosalia wakatoroka wakati wa kifungua kinywa wakati ambao maafisa wa usalama wanakua na shughuli nyingi.

Baadhi ya Wakenya wanaunga mkono hatua ya watu hao kutoroka kwenye kituo cha karantini. Mmoja wao ni Royn Kean ambaye kupitia mtandao wa Twitter anasema ''Ninawaunga mkon, unawezaje kunilazimisha kulipia karantini.

Post a Comment

0 Comments