Album ya Harmonize ‘Afro East’ yazidi kupaa

Miezi miwili na siku kadhaa zimepita toka kuachiwa kwa Album ya Afro East ya Harmonize imendelea kufanya vizuri kwenye mtandao wa Audiomack.
Mpaka sasa Album hiyo imesha sikiliza zaidi ya mara Milioni 6 kwa kipindi cha miezi miwili na kuifanya kuwa Album iliyosikilizwa zaidi kwenye mtandao huo kutoka nchi za Afrika Mashariki na kati.
Katika orodha hiyo Album ya Afro East inashikilia namba moja, huku namba mbili ikishikiliwa na Diamond Platnumz kupitia Album yake ya A Boy from Tandale.
A Boyo From Tandale ya Diamond Platnumz imesikilizwa zaidi ya Mara Milioni 5.77 na namba tatu inashikiliwa na Jux kupitia Album yake ya The Love Album iliyosikilizwa zaidi ya mara Milioni 5.72 kwenye mtadao huo.

Post a Comment

0 Comments