Baada ya mwanajeshi wa Ikulu kukutwa na corona, Trump apima tena asema hana corona


Rais wa Marekani Donald Trump na Makamu wake wa Rais Mike Pence wamelazimika kupima tena corona baada ya Mwanajeshi anayefanya kazi Ikulu kubainika ana corona, Trump na Pence wote ni wazima, hawajakutwa na virusi hivyo.

"Tuna vipimo bora kuliko Nchi zote Duniani, nimepima jana na leo pia na sina corona, kupima sio kitu kigumu, imenishangaza kuona Mtu wangu wa karibu ana corona namfahamu ni Mtu mzuri, ila ndio hivyo wasiwasi umetanda kila kona unaweza kukutana na Mtu ni mzima, kesho ukasikia tayari ana corona”- TRUMP

Post a Comment

0 Comments