Cardi B kuja na wimbo mpya

Mwanamuziki wa Marekani, Cardi B amefunguka na kuwataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kuupokea wimbo wake mpya baada ya kimya cha muda mrefu.
Cardi B aliwaambia mashabiki zake kwamba “Wimbo wangu mpya unakuja hivi karibuni. Sawa jamani?” aliwaambia watazamaji 80,000 waliohudhuria kwenye LIVE yake.
Ujio wa kazi hiyo mpya ya Cardi B umechukua muda mrefu na iliwahi kuripotiwa kwamba ni kutokana na sababu za kimakubaliano pamoja na label yake Atlantic Records, lakini inaonekana wamefikia muafaka.
Cardi hajaachia wimbo wowote tangu “Press” iliyotoka Mei 2019 na amekuwa akitudokeza pia kuhusu ujio wa album mpya tangu ‘Invasion of Privacy’ ya mwaka 2018.
Wiki iliyomalizika pia alituonesha tattoo yake mpya ambayo imeanzia shingoni na kupita kwenye kalio lake la kushoto hadi kwenye paja, imetajwa kutumia zaidi ya masaa 60 (Siku 2 na Nusu) kupaka hizo rangi na imemchukua miezi kadhaa kuikamilisha tattoo yote kwenye miji zaidi ya kumi.

Post a Comment

0 Comments