Iran yapuuzia madai ya Marekani

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Iran leo amepuuzia kile alichokiita kuwa ni "ujinga", madai ya Marekani kurefushwa vikwazo vya silaha vya Umoja wa Mataifa na kusema nchi hiyo inania ya kupuuzia hatua hiyo.

Matamshi ya kijinga ya Wamarekani sio kitu kipya, Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Mohammad Javad Zarif amesema leo, katika matamshi yaliyotolewa na shirika la habari la Isna.

Hususan iwapo madai hayo yanatoka kwa mtu ambaye amependekeza kunywa dawa ya kuosha mikono kuepuka maambukizi ya virusi vya corona, aliongeza, akimaanisha matamshi kutoka kwa rais Donald Trump mwezi uliopita.

Madai ya Marekani ambayo Zarif alikuwa akiyaeleza ni juhudi zinazohusiana na azimio la Umoja wa Mataifa namba 2231, ambamo baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa iliunga mkono makubaliano ya kinyuklia ya Iran yaliyotiwa saini mjini Vienna mwaka 2015.

Post a Comment

0 Comments