Obama aibuka kuwa mtu muhimu uchaguzi wa 2020

Karibu miaka minane baada ya kushiriki uchaguzi wa rais kama mgombea, Barack Obama anaibuka kama mtu muhimu katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2020.

Wanachama wa chama cha Democratic wanamtazama Obama kwa shauku kama mtu wa pembeni wa kisiasa wa Joe Biden, aliehudumu mihula miwili kama makamu wake wa rais.

Obama anasalia mtu maarufu zaidi katika chama cha democratic, hasa miongoni mwa wapigakura wenye asili ya Afrika na wanachama vijana wa Democratic, na timu ya kampeni ya Biden, inapanga kumpa jukumu la juu katika miezi ijayo.

Wakati Biden anatazamia kumtumia Obama kuimarisha nafasi yake, analenga pia kurejesha baadhi ya urithi wa Obama, ambao umevunjwa kwa maksudi na Trump, ambaye anawania kukamilisha kazi yake.

Post a Comment

0 Comments