Pompeo: Rais Trump kuchukua hatua dhidi ya wanafunzi wa China

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo amesema, Marekani itachukua hatua za kuzuia madai ya ujasusi unaofanywa na wanafunzi wa China, wakati kukisubiriwa tangazo litakalotolewa na rais Donald Trump.

Trump alisema kwamba atafanya mkutano na waandishi wa habari hii leo kuhusu China, katika wakati ambapo wasiwasi unaongezeka kati ya mataifa hayo mawili, ikiwa ni pamoja na suala ya hadhi ya Hong Kong na janga la COVID-19.

Pompeo alipoulizwa kuhusu ripoti ilyiitolewa na gazeti la New York Times kwamna Trump anaazimia kuwafurusha maelfu ya wanafunzi, alisema jana kwamba wanafunzi wa China hawatakiwi kuwa kwenye shule zetu kutuchunguza.

Ingawa hakusema kama Trump atatangaza hatuo hiyo leo, lakini alisema wanajua hiyo ni changamoto na ana uhakika kwamba Trump atalichukulia hatua.

Post a Comment

0 Comments