Rapa wa Uingereza afariki kwa ugonjwa wa corona

Rapa Ty wa Uingereza ambaye jina lake halisi ni Ben Chijioke amefariki baada ya kushambuliwa na virusi vipya vya corona (covid-19).

Taarifa za kifo cha rapa huyo zimethibitishwa na timu yake, ambayo imeeleza kuwa alifariki jana, Mei 7, 2020 akiwa hospitalini.

Imeelezwa kuwa Ty alikuwa amelazwa hospitalini katika chumba cha watu mahututi na alikuwa anasumbuliwa na maradhi yaliyoambatana na maambukizi ya virusi vya corona.

Rapa huyo aliyekuwa na umri wa miaka 47 hivi karibuni alikuwa miongoni mwa waliotajwa kuwania tuzo ya ‘Mercury’ kupitia albam yake ya ‘Upwards’.

TY aliingia kwenye mkondo mkuu wa kiwanda cha burudani mwaka 2001 alipoachia albam yake ya kwanza ‘The Awkward’, mwaka 2004 albam yake ‘Upwards’ ilitajwa kuwania tuzo za ‘Mercury’.

Post a Comment

0 Comments