Sherehe za kukabidhi kombe la Ubingwa ligi kuu ya Uingereza kufanyika kama kawaida

Mtendaji Mkuu wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza Richard Masters ametangaza kuwa sherehe za kukabidhi kombe kwa bingwa wa ligi hiyo zitafanyika kama ilivyo desturi ya kumtangaza bingwa, japokuwa kwa mwaka huu itakuwa chini ya uangalizi maalum.

Masters amesema shughuli hiyo ni lazima kwa mujibu wa kanuni zinazosimamia uendeshaji wa ligi ambazo zinawatendea haki wachezaji na viongozi wa timu washindi ambar wametoa jasho hadi kupata mafanikio hayo.

Kipekee amewataja Liverpool ambao kwa mujibu wa hesabu wananafasi kubwa ya kutwaa ubingwa huo, akisema wanahitaji kupata ushindi kwenye mechi mbili pekee ili wachukue ubingwa ambao wameuwinda kwa miaka 30 sasa.