Tommy Flavour akanusha kuwakimbiza Killy na Cheed

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Tommy Flavour kutoka Kings Music Records amekanusha tuhuma zinazodaiwa kwamba uwepo wake ndani ya lebo hiyo, umesababisha wasanii Killy na Cheed kuondoka.
msanii huyo amesema yeye ndiyo amepitia kipindi kigumu kuliko wengine na suala la kuondoka kwao haihusiani na yeye, kwani kila mtu alipewa nafasi yake.
“Taarifa za kuondoka kwao zilinipata nikiwa nyumbani na niliziona mitandaoni wakiwazungumzia, sikuwa na ubaguzi na wote walikuwa washkaji zangu na Kings ilitoa nafasi kwa kila msanii.
Amesema mimi sio sababu ya wao kutoka kwanza mimi ndiyo nilipitia kipindi kigumu zaidi, maana nimechelewa kutoa kazi na kuna mambo yalitokea kwahiyo kama ingekuwa wa kukasirika basi ningekuwa mimi”.
Msanii anatamba na wimbo wake Omukwano aliofanya na mwanamuziki Alikiba ambaye ni boss wake.

Post a Comment

0 Comments