TOP STORIES Wafungwa 100 wapata Corona DRC

Taarifa ya hivi karibuni kutoka Wizara ya Afya mjini Kinshasa inasema kuwa visa 101 vya COVID-19 vimethibitishwa katika gereza hilo la kijeshi, ingawa 92 kati ya walioambukizwa walikuwa katika hali nzuri.
Kumbukumbu za kikao cha baraza la mawaziri ambazo nakala yake imeonekana na shirika la habari la AFP, zimesema maambukizo hayo yanaweza kuwa kitisho kikubwa kwa jamii, hususan ikiwa yataenea hadi gereza la Makala lenye msongamano mkubwa wa wafungwa.
Kumbukumbu hizo zimesema kwa kuzingatia jinsi maambukizi yalivyosambaa kwa kasi katika gereza la kijeshi la Ndolo, uwezekano wa kulifikia gereza la Makala hauwezi kupuuzwa

Post a Comment

0 Comments