Vita vya kibiashara Marekani na China vyaendelea, masoko ya hisa New-York yaporomoka

Masoko ya hisa New-York yameporomoka leo Jumatatu baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kusababisha hofu kutokana na hatua ya kuanzisha tena vita vya kibiashara na China kufuatia dhima yake katika janga la virusi vya Corona
Madai yanayotolewa na Rais huyo wa Marekani na Waziri wake wa Mambo ya Nje Mike Pompeo kwamba ugonjwa huo ulianzia kwenye maabara moja ya mjini Wuhan, China na kwamba waliohusika watabeba dhamana, yamegubika hatua za kuzuia kutokea maambukizi zaidi na vifo kutokana na ugonjwa wa Covid-19.
Rais Trump amesema huenda akatangaza viwango vipya vya ushuru dhidi ya China kutokana na jinsi inavyolishughulikia janga la mlipuko wa virusi vya Corona, akidai kwamba ameona ushahidi unaoihusisha maabara ya Wuhan na janga hilo.
Kuporomoka kwa masoko ya hisa kote barani Asia kumekuja wakati wawekezaji wakirejea baada ya kurefushwa kipindi kufungwa biashara.

Post a Comment

0 Comments