Alichoongea Uchebe kuhusu ndoa yake na Shilole

 

Aliekuwa mume wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shilole aitwae Ashraf Uchebe amefunguka mambo aliyopitia akiwa na Shilole.

Uchebe amesema kuwa hawezi kusema ndoa ni mbaya kwa sababu ni jambo la kheri, sisi ni vijana bado tunakutana na mambo mengi, kwanza mimi nimepita kwenye ndoa ya kwanza kwa binti mwenye miaka 16, wapili ndiyo huyu.

Ameendelea kusema kuwa anapopatwa na matatizo huwa anamuomba sana Mungu asifanye jambo la ajabu, maana wanawake wana vitu viwili kwanza anapomkosea mumewe hakubali anataka kushindana naye, na kwenye ndoa wanawake ndiyo inawabeba sana.

Pia ameendelea kusema kuwa muda mwingine bora tutumie washenga ambao ni watu wazima, nahisi nilikosea kutumia mshenga ambaye kijana mwenzangu na sitarudia tena, kwanza yule mshenga nimempotezea, mimi najiamini kuliko kitu chochote ndiyo maana naambiwaga nina jeuri

Ameongeza kwa kusema kuwa mitahani ipo na inatokea ni moja ya hatua kwenye maisha sasa hivi nimejipunguza kidogo sipo karibu na mwenzangu, nimetoa talaka ambazo zina awamu na anatakiwa akae heda na kupata huduma, ukitaka kuoa kuna misingi mingi unatakiwa kuifuata”

Mwisho amemalizia kwa kusema kuwa taarifa kuhusu kesi kuwa mahakamani zipo na zitaendelea kuwepo, unajua unapokutana na mwanamke mwenye mapungufu lazima uwe na subira, pia kheri inabidi uitangaze na shari inatakiwa ifichwe.

Post a Comment

0 Comments