Baraka The Prince akanusha kutumia uchawi katika kazi zake


 Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Baraka The Prince amefunguka kuhusu suala zima la wasanii kujihusisha na mambo ya kishirikina katika muziki wao kama njia moja wapo ya kutaka kufanikiwa au kutoboa kwenye muziki.

Baraka The Prince amesema kuwa katika maisha yake ya muziki hakuwahi kutumia ushirikina japokuwa wengine wanafanya hivyo.

Baraka The Prince ambaye anasifika kwa nyimbo za mapenzi amesema kuwa kwa upande wake hana imani na mambo ya kishirikina na anamuamini Mungu kama mganga wake mkuu katika muziki.

“Siamini sana mambo ya ushirikina na sijawahi kufanya nasikiaga tu watu wanasema ila nimeweza kufanikiwa bila kwenda kwa waganga mimi mganga wangu mkuu ni Mungu mwanadamu mwenzangu atawezaje kunifungulia mambo naamini sana katika sala na Mungu”.

Mwanamuziki huyo kwasasa anatamba na wimbo wake mpya unaokwenda jina la Sawa ambao ameuachia hivi karibuni

Post a Comment

0 Comments