Harmonize awapa somo wasanii wake wapya


 Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amewataka wasanii wake wapya Cheed na Killy kuzingatia nidhamu kwani ndiyo silaha ya mafanikio ndani ya lebo ya Konde Gang.

Harmonize kupitia akaunti ya lebo ya Konde Gang amewatambulisha wasanii hao kuwa chini yake baada ya kuachana na lebo ya Kings Music chini ya Alikiba.

Harmonize amewakaribisha na kuwapaa maneno yenye kuwatia moyo kwa kuwaambia kuwa Konde Gang ni lebo kubwa na silaha yao ni nidhamu, upendo na kufanya kazi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize ameandika “Brothers 4 REVER, karibuni Killy na Cheed, silaha yetu ni upendo pamoja na kazi maana hizo ndiyo haja za wananchi wanaoifanya leo hii Konde Gang Music kuwa ulimwenguni, Konde Gang ni rekodi lebo kubwa.

Konde Gang itakuwa na jumla ya wasanii watano mpaka sasa ambao ni Harmonize, Young Skales, Ibrah , Killy pamoja na Cheed

Post a Comment

0 Comments