Kwa wale wafuatiliaji wa filamu hawatakuwa wageni wa jina la ‘Steven Frederic Seagal’ aliyezaliwa Aprili 10 mwaka 1952 eneo la Lansing Michigan, nchini Marekani. Mbali na sanaa ya uigizaji, Seagal pia ni Mwanamuziki, mtunzi na muandaaji wa filamu na afisa polisi wa kitengo cha dharura cha Sherriff. Leo anasharekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza nyundozz 62 duniani.
Staa mwingine aliyezaliwa tarehe na mwezi kama wa leo ni mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Brazil na Real madrid, ‘Roberto Carlos da Silva Rocha’ aliyezaliwa miaka 41 iliyopita katika jiji la Sao Paulo, kitongoji cha Garca nchini Brazil..
Blogu ya Larrybway91 inawatakia maisha marefu Seagal, Carlos na kwako wewe mtembeleaji wa blogu yetu ambaye umezaliwa tarehe na mwezi kama wa leo. Happy Birthday to you
0 Comments