Killy na Cheed wajiunga Konde Gang ya Harmonize

 

Baada ya kuachana na King Music, Wasanii wa Bongo Fleva, Killy na Cheed wamejiunga rasmi na lebo ya muziki nchini Konde Gang inayomilikiwa na msanii wa Bongo Fleva, Harmonize.

Wasanii hao wametangaza kwa pamoja kupitia kurasa zao za mtandao wa Instagram, huku wakimshukuru boss wao wa zamani Alikiba kwa kuwaonyesha njia na kuwaamini kufanya nao kazi.

Killy kupitia akaunti yake Instagram ameandika “Siwezi kumsahau kaka angu aliyenilea, akaniamini na kunishika mkono na kuniaminisha zaidi kwa watanzania hasa kwa mashabiki wa Bongo Flavour, na kunionyesha njia katika kipindi chote tulichokuwa pamoja kaka angu Alikiba”

Pia ameandika “Napenda kuwataarifu mashabiki zangu na watu wote wanaosupport kazi zangu kiujumla tangu hapo awali mpaka hapa nilipofikia, nawajulisha kuwa kijana wenu nimejiunga rasmi na kampuni ya uzalishaji na usimamizi wa muziki Tanzania Konde Gang”.

Cheed na Killy walijitoa Kings Music mwezi Aprili, hivyo wataungana na wasanii kama Ibrah Tz, Young Skales kwenye lebo ya Konde Gang ambayo inasimamiwa na Harmonize

Post a Comment

0 Comments