Mwanamuziki wa Zimbabwe atamani kufanya kazi na Harmonize

 

Mwanamuziki kutoka nchini Zimbabwe, King 98 amefunguka kuhusu kufanya collabo na msanii na Boss wa Konde Gang, Harmonize.

King 98 amesema hakuna shida kufanya kazi na Harmonize kwa sababu hata nchini kwao Zimbabwe wapenzi wa muziki wanamkubali sana.

“Kufanya collabo na Harmonize sio kitu kibaya, na kizuri zaidi ni msanii mkubwa  ambaye hata nchini kwetu watu wanamkubali hivyo ningependa nifanye nae kazi” amesema King 98

Aidha akizungumzia kuhusu maisha yake binafsi nje ya muziki King 98 ameeleza kuwa “Vitu ninavyopata maishani mwangu ni Baraka.

Pia amesema kuwa siwezi kuwapa watu nafasi kwa ajili ya vitu vingine nafanya kazi ili watu waone, muda wangu mwingi natumia kwa ajili ya mama yangu, na  mpenzi wangu na mtu ambaye  ananishawishi ni baba yangu”

Post a Comment

0 Comments