Sababu ya Diamond kuimba kidogo kwenye wimbo wa Alicia Keys


 Mtayarishaji wa muziki nchini Marekani, Swizz Beatz amelazimika kutoa sababu ya kwa nini mwanamuziki Diamond Platnumz ameimba kidogo kwenye wimbo aliofanya na Alicia Keys wa Wasted Energy.

Swizz Beatz amekuwa akipitia na kujibu maoni mbalimbali juu ya albam mpya ya mwanamama huyo ALICIA, ambayo ndani yake anapatikana Diamond.

Swizz Beatz alilazimika kufunguka kwenye moja ya komenti katika ukurasa wa Alicia Keys wa Instagram, ambapo aliandika;

“My brother for life, please let your fans know you did as you pleassed on the record and this is just part one”.

Baadhi ya mashabiki wamemtaka Diamondi kujitokeza hadharani na kufafanua juu ya ishu hiyo, kwani Wabongo wamekuwa wakitumia lugha isiyokuwa ya staha katika kumshambulia Alicia Keys, jambo ambalo linaweza kuharibu taswira ya wasanii wa Bongo Fleva huko ughaibuni.

Post a Comment

0 Comments